Tenzi za Rohoni – 31

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MSINGI IMARA

1.Msingi imara, enyi wa kweli,
Umekwisha pigwa kwa neno hili;
Aongeze lipi? Mnayo pia
Kwa Yesu mliomkimbilia.

2.Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka taipunguza;
Takupa nawe, nikuwezeshe,
Ipata kufaa, isikutishe!

3.Utakapopishwa ndani ya moto
Nnguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.

4.Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni kwisha mapenzi yangu;
Nazo zitakapowenea, ndipo
Mabegani mwangu niwatwekapo.

5.Na mtu aliyenitegemea
Kamwe kwa adui sitamtia;
Nguvu za jehanam zijapotisha,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi