Tenzi za Rohoni – 34

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NJONI WENYE DHAMBI

1.Njoni! Njoni! Wenye dhambi,
Njoni, msikawie;
Yesu awangojea ndiye awapendaye;
Ajuaye awezaye
kuwaponya ni Yeye.

2.Ewe muhitaji uje;
Anakukaribisha,
Imani, kweli, na toba,
Neema ya kutosha,
Jua sana, kwake Bwana
Bure utapata.

3.Njoni, mliolemewa
Na dhambi ya Adamu;
Mkingoja kujiponya
Mtapotea mumu;
Si wa haki, ni wakosa
Waoshwao kwa damu.

4.Ikamtokea dhiki,
Mle Gethisemani;
Kisha alipoangikwa
Akalia mtini;
” Imekwisha”, alitosha
Dhabihu ya thamani.

5.Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea huko;
Basi mtumai yeye;
Kamwe mwingine hako
Yesu pweke, Yesu pweke,
Ndiye Mwokozi wako.

6.Wamsifu-sifu sana
Mbinguni malaika;
Wachanganya nyimbo zao
Na waliookoka:
Aleluya wataimba
Waliooshwa taka.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi