Tenzi za Rohoni – 37

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

WAITWA, MWOVU, NA BWANA

1.Waitwa, mwovu, na Bwana
Umwendee hima sana,
Usafiwe dhambi zako,
Humwoni ni mwema kwako?

Unaitwa! Itika tu!
Umwendee Bwana Yesu!
Sifiche makosa yako,
Uungame dhambi zako!
Kristo tu umuamini,
Ndiyo njia ua Mbinguni.

2. Alilipa damu yake
Ili kukukweza kwake;
Alikufa yeye Bwana,
Mimi nawe tuwe wema.

3.Ukifanywa kuwa mwema
Mwishoni utasimama,
Utaingia rahani
Na wapenzi wa zamani.

4.Ni mwanga tu, nchi ile;
Uovu hauko kule,
Kwamba wataka ufike
Sharti huku uosheke.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi