Tenzi za Rohoni – 38

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWENDE KWA YESU

1.Twende kwa Yesu mimi nawe,
Njia atwonya tuijue
Imo Chuoni; na Mwenyewe,
Hapa asema, Njoo!

Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako, Mwokozi, kuonana,
Na milele kukaa.

2. ”Wana na waje”, atwambia,
Furahini mkisikia,
Ndiye mfalme wetu pia,
Na tumtii, Njoo.

3. Wangojeani? Leo yupo;
Sikiza sana asemapo;
Huruma zake zikiwapo,
Ewe kijana, Njoo.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi