Tenzi za Rohoni – 39

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MWENYE DHAMBI HUNA RAHA

1.Mwenye dhambi huna raha,
Sikiza nakusihi,
Utapata msamaha
Kwake Yesu Mwokozi!
Njoo hima, njoo hima,
Naye atafurahi.

2. Yesu anakwita sana
Naye yuko Mbinguni;
Hofu ya kifo hapana
Kwake ukiamini.
Njoo hima, njoo hima,
Utapata amani.

3. Hatakwita siku zote;
Ni ya sasa nafasi.
Lete na uchafu wote,
Kukawa haipasi.
Njoo hima, njoo hima,
Ni wokovu halisi.

4.Uzima uko kwa Bwana
Twae uzima hasa
Bure unapatikana,
Wokovu twae sasa!
Njoo hima, njoo hima,
Twae utakatifu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi