Tenzi za Rohoni – 41

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

YESU ALINIITA, “NJOO”

1.Yesu aliniita, “njoo,
Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze
Kifuani mwangu.”
Nilikwenda kwake mara,
Sana nilichoka;
Nikapata kwake raha,
Na furaha tena.

2. Yesu aliniita, “njoo,
Kwangu kuna maji,
Maji ya uzima, bure,
Unywe uwe hai, ”
Nilikwenda kwake mara
Na maji nikanywa:
Naishi kwake, na kiu
Kamwe sina tena.

3.Yesu aliniita, “njoo,
Dunia ni giza,
Ukinitazama nuru
Takung’arizia.”
Nilikwenda kwake mara
Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga
Safarini mwangu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi