Tenzi za Rohoni – 44

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KUKAWA NA GIZA DUNIA YOTE

1.Kukawa na giza dunia yote,
Ni Mwanga wa ulimwengu,
Ikaisha ulipokuja yote,
Ni mwanga wa ulimwengu.

Jua, Yesu hana mwenziwe!
Nalipofuka kama wewe:
Nakuombea umwone nawe,
Ni mwanga wa ulimwengu.

2.Hatuna giza tudumuo mwake,
Ni mwanga wa ulimwengu;
Tumwandamiapo nyayoni mwake
Ni mwanga wa ulimwengu.

3.Enyi wa gizani wenye kutanga!
Ni mwanga wa ulimwengu,
Kaulekeeni, mpate lenga;
Ni mwanga wa ulimwengu.

4.Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu
Ni mwanga wa ulimwengu:
Ni nuru za mbingu kondoo wa Mungu
Ni mwanga wa ulimwengu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi