Tenzi za Rohoni – 45

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MTAZAME HUYO! ALIYEANGIKWA JUU

1.Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu
Wala usifanye tashwishi.

Tazama! Tazama! Tazama uishi!
Mtazame huyo aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.

2.Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi,
Na makosa yako maovu!
Kama deni zetu zote hakulipa
Mbona imemwagika damu?

3.Si kutubu na sala ikomboayo,
Ila damu ndiyo salama;
Na aliyeimwaga aweza, sasa,
Dhambi zako kukufutia.

4.Usiwe na shaka, Mungu amesema,
Hakuna alilolisaza;
Hapo alipokuja alitimiza
Kazi zote alizoanza.

5.Basi twae uzima, kwa kufurahi
Upokee kwa Bwana, sasa;
Ujijue hakika kwake kuishi
Yesu aishiye kabisa.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi