Tenzi za Rohoni – 46

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWAE WANGU UZIMA

1.Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku,
Zikutukuze huku.

2.Twae mikono nayo
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu.

3.Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.

4.Twae dhanabu pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.

5.Nia itwae, Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako.

6.Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Nniwe wako halisi.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi