Tenzi za Rohoni – 47

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NI WAKO WEWE

1.Ni wako wewe, nimekujua,
Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea.

Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Sana, kwako mtini.
Bwana vuta, vuta, nije nisongee,
Pia damu ya thamani.

2.Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende,
Nizidi kukwandama.

3.Nina furaha tele kila saa
Nizungumzavyo kwako,
Nikuombapo nami napata kujua nia yako.

4.Mapenzi yako hayapimiki,
Ila ng’ambo ya liko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi