Tenzi za Rohoni – 48

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NAWEKA DHAMBI ZANGU

1.Naweka dhambi zangu
Juu yake Bwana
Kuziondoa, kwangu
Hulemea sana;
Na uaili wangu
Ameuondoa;
Dawa yangu ni damu,
Kwa hiyo napoa.

2.Na uhitaji wangu
Nitamjuvisha
Kwa upungufu wangu
Yeye anatosha;
Majonzi yangu yote
Na mizigo yangu,
Atachukua vyote
Yesu Bwana wangu.

3.Na roho yangu nayo,
Imechoka sana;
Namletea hiyo
Ilindwe na Bwana;
Ni jema jina lake,
Nalo lapendeza,
Imanweli na kwake
tutalitukuza.

4.Natamani daima
Niwe kama Bwana,
Mpole, tena mwema,
Wa mapenzi sana;
Zaidi natamani
Kwenda kwake juu,
Nikaone mbinguni
Enzi yake kuu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi