Tenzi za Rohoni – 49

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NITWAE HIVI NILIVYO

1. Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu,naja,naja.

2.Hivi nilivyo;si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu,naja,naja.

3.Hivi nilivyo; sioni
Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu,naja,naja.

4. Hivi nilivyo kipofu,
maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu;
Bwana Yesu,naja,naja.

5.Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu,naja,naja.

6. Hivi nilivyo;mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu,naja,naja.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi