Tenzi za Rohoni – 50

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

YESU NAKUPENDA, U MALI YANGU

1.Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

2.Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

3.Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

4.Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

5.Mawanda mazuri, na masikani
Niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi