Tenzi za Rohoni – 52

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

YOTE NAMTOLEA YESU

1. Yote namtolea Yesu
Nampa moyo wote,
Nitampenda siku zote,
Namwandama kila saa.

Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee mwokozi,
Natoa sasa.

2. Yote namtolea Yesu,
Nainamia pake;
Nimeacha na anasa,
Kwako Yesu nipokee,

3. Yote namtolea Yesu,
Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana,
Anilinde daima,

4. Yote namtolea Yesu,
Nami naona sasa;
Furaha ya ukombozi,
Nasifu jina lake,

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi