Tenzi za Rohoni – 54

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

YESU NATAKA KUTAKASWA SANA

1.Yesu nataka kutakaswa sana,
Nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka
Unioshe sasa niwe mweupe.

Mweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.

2.Bwaba Yesu, unitazame sasa,
Unifanye niwe dhabihu hai;
Najitoa kwako, na moyo wote;
Unioshe sasa niwe mweupe.

3.Bwana kwa hiyo nakuomba sana,
Nakungojea miguuni pako,
Naomba unioshe damuni tu,
Unioshe sasa niwe mweupe.

4.Bwana nidumu kukungojea,
Niumbie moyo safi, Ee Mungu,
Wanaokujia hutupi kamwe,
Unioshe sasa niwe mweupe.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi