Tenzi za Rohoni – 55

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NIPE MOYO WENYE SIFA

1.Nipe moyo wenye sifa
Sio wa utumwa;
Moyo ulionyunyizwa
Damu ya thamani.

2.Moyo msikizi, moyo
Wa kunyenyekea,
Moyo utawaliwao
Na Mwokozi pia.

3.Mwenye kutubu, mnyonge,
Sadiki, amini;
Kamwe, kamwe asitengwe
Akaaye ndani.

4.Mpya, mwema na mawazo
Mwingi wa mapenzi
Nawe uwe kielelezo
Moyo wa Mwokozi.

5.Ni uule moyo wako;
Moyo wa huruma
Yesu, natamani kwako
Kukujua vyema.

6.Na ya midomo matunda
Yako, nipe nami;
Amani isiyokoma
Iwe yangu mimi.

7.Nitie yako tabia,
Inishukie juu;
Jina lako nipe pia,
Ndilo la upendo.

8.Ni wa baba utukufu;
Mwana atukuke;
Na roho Mtakatifu
U utatu pweke.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi