Tenzi za Rohoni – 57

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NAENDEA MSALABA

1.Naendea Msalaba,
Ni mnyonge na mpofu,
Yapitayo naacha,
Nipone Msalabani.

Nakutumaini tu,
Ewe Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako;
Niponye, mponya wangu.

2.Nakulilia sana:
Nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema;
“Nitazifuta zote”.

3.Natoa vyote kwako,
Nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili,
Viwe vyako milele.

4.Kwa damu yake sasa,
Nimegeuka roho,
Nikaziacha tama
Nimfuate Yesu tu.

5.Yesu yuaja tena!
Nimepevuka kwake,
Kila chembe kamili;
Msifuni yeye mponya!

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi