Tenzi za Rohoni – 58

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MWAMBA WENYE IMARA

1.Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha!
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.

2.Kwa kazi zote pia ,
Sitimizi sharia.
Nijapofanya bidii,
Nikilia nakudhii,
Hayaishi makosa;
Ndiwe wa kuokoa.

3.Sina cha mkononi,
Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike;
Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.

4.Nikungojapo chini,
Nakwenda kaburini;
Nipaapo Mbinguni,
Na kukwona enzini:
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi