Tenzi za Rohoni – 59

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

PELELEZA NDANI YANGU

1.Peleleza ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako Mungu,
Idhihiri pia.

2.Peleleza moyo wangu
Uunifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.

3.Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi
Ni la kuchukiza.

4.Peleleza na mawazo
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo – umbo.

5.Zidi kuyapeleleza
Katikati yangu
Hata wishe nifundisha
Udhaifu wangu.

6.Hapo nikikwinamia
Mbele zako, Mungu,
Hakika nitakujua
U mpenzi wangu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi