Tenzi za Rohoni – 64

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

UJARIBIWAPO, SIFANYE DHAMBI

1.Ujaribiwapo, sifanye dhambi,
Bali uzishinde, kwa Yesu kutii.
Fuliza kiume ushinde tamaa;
Yesu ni Mwokozi, hukuokoa.

Umwombapo yu papo
Akuongeze nguvu,
Atakusaidia;
Yesu atakufaa.

2.Wepushe waovu, matusi dharau;
Heshima la Mungu, kamwe sisahau;
Fanya uhodari, uwe mpole,
Atakuokoa hata milele.

3.Avumiliaye hupewa taji;
Tujaposumbuka tu washindaji,
Na mwokozi wetu hutuwezesha
Tusiwe kushindwa kama twakesha.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi