Tenzi za Rohoni – 67

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

BWANA ULIYEWAITA

1.Bwana uliyewaita
Watakatifu wako,
Wawe mitume, wachunga,
Walishe kundi lako;
wanyonge na wenye hofu
Wakawa mashujaa,
Na wapole wa kunena
Wasiwe kunyamaa.

2.Hata leo wawataka
Watakatifu wako,
Nawe wauliza tena
Ni nani aliyeko
Atakaye nimtume
Afundishe vijana?
“Ni tayari, Bwana wangu,
Nitume mimi Bwana.”

3.Nitume na mimi, Bwana
Kama ulivyotumwa,
Habari ya msamaha
Na dhambi kutubiwa,
Niwahubiri wakosa,
Na waliopotea,
Wokovu u wake Bwana,
Aliyewafilia.

4.Astahiliye hapana
Kutamka habari,
Lakini wewe waweza
Kutufanya tayari.
Neno lako tulijue,
Tupe na roho yako,
Hayatakuwa ya bure,
Haya maneno yako.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi