Tenzi za Rohoni – 68

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MUNGU MSAADA WETU

1.Mungu msaada wetu
Tangu myaka yote,
Ndiwe tumaini letu
La zamani zote.

2.Kivuli cha kiti chako
Ndiyo ngome yetu.
Watosha mkono wako
Ni ulinzi wetu.

3.Kwanza havijakuwako
Nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako
Twakaa salama.

4.Na myaka elfu ni kama
Siku moja kwako;
Utanilinda daima
Tu wenyeji wako.

5.Binadamu huondoka,
Mwisho hana kitu;
Kama ndoto hutoweka
Ndivyo hali yetu.

6.Ila wewe Mungu wetu
Ndiwe wa kudumu;
Ndiwe bora, ngome yetu
Twakaa dawamu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi