Tenzi za Rohoni – 69

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWENDENI ASKARI

1.Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.

Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

2.Jeshi la Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia,
Kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu inueni zenu sauti.

3.Kweli kundi dogo, watu wa Mungu
Sisi na mababa tu moja fungu.
Hatutengwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.

4.Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi