Tenzi za Rohoni – 72

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWENDENI! HARAKA!

1.Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza.
Bwana alisema nendeni po pote
Kawafundisheni mataifa yote.
Pelekeni Injili kwa jina la Yesu.
Upesi! Twendeni haraka!

2.Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
La upendo wa Mungu kwa watu wote;
Aliyeupenda sana ulimwengu
Akamtoa Yesu Mwana wake pekee
Kaleta wokovu, tumtangazeni.
Upesi! Twendeni haraka!

3.Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
La uzima kwa watu waliokufa.
Mateka ya Shetani litafungua
Litaponyesha na kuwapa amani.
Twendeni upesi, tukawaokoe.
Upesi! Twendeni haraka!

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi