Tenzi za Rohoni – 75

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

WAIMBA, SIKIZENI

1.Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni;
Wimbo wa tamu sana
Wa pendo zake Bwana,
“Duniani salama,
Kwa wakosa rehema.”
Sisi sote na twimbe
Nao wale wajumbe;
Waimba, sikizeni,
Malaika mbinguni.

2.Ndiye Bwana wa Mbingu,
Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili,
Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini
Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie,
Ili tusipotee.
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.

3.Mtukufu wa amani
Ametoka Mbinguni,
Jua la haki, ndiye
Atumulikiaye;
Amejivua enzi,
Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya,
Kutuzalisha upya,
Waimba sikizeni,
Malaika Mbinguni.

4.Njoo upesi, Bwana,
Twakutamani sana;
Kaa nasi, mwokozi
Vita hatuviwezi;
Vunja kichwa cha nyoka,
Sura zako andika,
Tufanane na wewe,
Kwetu sifa upewe,
Waimba, sikizeni,
Malaika Mbinguni.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi