Tenzi za Rohoni – 76

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NJONI, ENYI WA IMANI

1. Njoni na furaha, enyi wa imani,
Njoni Bethilehemu upesi !
Amezaliwa jumbe wa Mbinguni;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

2. Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga,
Amekuwa radhi kuzaliwa;
Mungu wa kweli, wala si kiumbe;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

3. Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu,
Mbingu zote na zijae sifa;
Sifuni Mungu aliye Mbinguni;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

4. Ewe Bwana mwema, twakubarikia,
Yesu, utukufu uwe wako;
Neno la Baba limekuwa mwili;
Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi