Tenzi za Rohoni – 79

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MSALABA WA AIBU

1.Msalaba wa aibu,
Ulinipa amani;
Uliniondoa kifungoni,
Nilimotesekea.

2.Ee, Mwokozi wangu, Yesu
Nitamwendea nani?
Najiweka msalabani,
Nikaoshwe damuni.

3.Nakupenda Bwana Yesu,
Kwa kunipenda kwako,
Napendezwa nikutumikie
Maisha yangu yote.

4.Usifiwe Bwana Yesu,
Kwa ulivyonifia,
Aleluya, nakushukuru,
Uliyenikomboa.

5.Msalaba ulishinda
Nguvu zake adui,
Ili mimi nikombolewe,
Niwe mwana wa Mungu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi