Tenzi za Rohoni – 80

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA

1.Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je neema yake umemwagiwa,
Tumeoshwa kwa damu ya kondoo?

Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

2.Wamwandama daima mkombozi
Na kuoshwa na damu ya kondoo?
Yako kwa msulubiwa makazi,
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

3.Atakapokuja Bwana –arusi
Uwe safi kwa damu ya kondoo!
Yafae kwenda mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya kondoo.

4.Yatupwe yaliyo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya kondoo.
Huoni kijito chatiririka
Na uoshwe kwa damu ya kondoo?

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi