Tenzi za Rohoni – 82

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

SIONI HAYA KWA BWANA

1.Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara!

Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.

2.Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi,
Alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi.

3.Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.

4.Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi