Tenzi za Rohoni – 84

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NIWONAPO MTI BORA

1.Niwonapo mti bora
Kristo aliponifia
Kwangu pato ni hasara
Kiburi nakichukia.

2.Na nisijivune, Bwana
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Ni chini ya damu yako.

3.Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimia.

4.Vitu vyote vya dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zinawia
Nafsi, mali, na maisha.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi