Tenzi za Rohoni – 85

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NI “MTU WA SIMANZI”

1.Ni “Mtu wa Simanzi”,
Mwana wa mwenye enzi
Mwenye mengi mapenzi!
Asifiwe Bwana Yesu!

2.Akawa matesoni,
“Mungu mwana yakini
Akatoka Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!

3.Akapata dhihaka,
Mzoea – mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Asifiwe Bwana Yesu!

4.Tu wenye dhambi sana;
Kwake dhambi hamna,
Na Mungu twapatana:
Asifiwe Bwana Yesu!

5.Alikufa mtini,
Akalia dhikini,
Sasa yuko Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!

6.Punde atarejea,
Yesu kutunyakua,
Ndipo tutamwimbia:
Asifiwe Bwana Yesu!

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi