Tenzi za Rohoni – 86

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

DAMU IMEBUBUJIKA

1.Damu imebubujika,
Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka,
Husafiwa kweli.

2.Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru,
Yanisafi ndani.

3.Kondoo wa kuuawa,
Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa,
Kwa utimilivu.

4.Bwana tangu damu yako
Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako;
Taimba milele.

5.Nikifa tazidi kwimba
Sifa za wokovu
Ulimi ujaponyamaa
Vumbini mwa ufu.

6.Bwana, umenikirimu
Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu
Ya mali ya kweli.

7.Nikubali kukwimbia,
Mbinguni milele,
Mungu nitakusifia
Jina lako pweke.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi