Tenzi za Rohoni – 87

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

1.Deni yangu ya dhambi,
Yesu amelipa.
Kwake msalabani
Nilipewa uzima.

Deni ya dhambi,
Msalabani,
Ilimalizikia,
Ni huru kabisa.

2.Bwana Yesu asema,
“Mwanangu dhaifu,
Uwezo wa ushindi
Hupatikana kwangu.”

3.Bwana, kweli naona,
Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma,
Niwe kipya kiumbe.

4.Sina wema moyoni,
Nidai neema,
Nakubali kabisa,
Kwa damu kusafiwa.

5.Hata huko Mbinguni
Miguuni pake,
“Yesu alinifia,”
Nitaimba milele.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi