Tenzi za Rohoni – 88

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NDIYO DAMU YA BARAKA

1.Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa,
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.

2.Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho,
Nami ni safi kabisa.

3.Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa;
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe kwa damu yako,
Nami ni safi kabisa.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi