Tenzi za Rohoni – 92

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NATAKA NIMJUE YESU

1.Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake, na
Wokovu wake kamili.

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake, na
wokovu wake kamili.

2.Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.

3.Nataka nifahamu, na
Nizidi kupambanua
Mapenzi yake, nifanye
Yale yanayompendeza.

4.Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi