Tenzi za Rohoni – 95

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

HIVI VITA VIMEKOMA

Aleluya! Aleluya! Aleluya!

1.Hivi vita vimekoma,
Vimeshindwa na uzima,
Na asifiwe daima,
Bwana Yesu.

2.Nguvu za kifo ni hizo,
Ila hazina uwezo,
Ndizo sasa avunjazo,
Bwana Yesu.

3.Siku tatu za huzuni,
Kisha atoka ufuni,
Asifiwe duniani,
Bwana Yesu.

4.Mapingu ameyavunja,
Mbingu amezifungua,
Nasi sasa twamwimbia,
Bwana Yesu.

5.Na ulivyopigwa wewe,
Ni kwamba tufunguliwe,
Milele na usifiwe,
Bwana Yesu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi