Tenzi za Rohoni – 96

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MLE KABURINI, YESU MWOKOZI

1.Mle kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa chini, Bwana wangu!

Bwana! Amefufuka,
Kifo kimeshindwa kabisa!
Gizani mle alitoka chini,
Sasa atawala huko Mbinguni!
Yu hai! Yu hai!
Bwana Yesu yu hai!

2.Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana ujao, Bwana wangu!

3.Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure ni muhuri, Bwana wangu!

4.Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi!
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu!

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi