Tenzi za Rohoni – 97

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TAZAMENI HUYO NDIYE

1.Tazameni huyo ndiye,
Mwenye kushinda vita;
Haya, tumsujudie;
Nyara anazileta;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.

2.Msifuni malaika,
Mtukuzeni sana,
Wote waliookoka
Watamsifu Bwana;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo kitini.

3.Walimfanya dhihaka
Zamani wenye shari,
Kwao waliookoka
Ni Bwana wa fahari;
Watu wote msifuni.
Sasa yumo Kitini.

4.Nyimbo nzuri, sikizeni,
Ni nyimbo za sifa kuu,
Za Bwana Yesu kitini,
Kutawazwa, yeye tu;
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi