Tofauti kati ya Ufalme na Demokrasia

Yesu tunaye mwamini na kumtumikia yeye ni mfalme, utawala wake wote ni wa kifalme. Sisi tumezaliwa na kukulia kwenye utawala wa kidemokrasia na  mifumo ya utawala wa kidemokrasia  iko tofauti kabisa na ya Ufalme. Ndiyo maana waamini wengi sana wanapita katika mazingira magumu sana ya kumtumikia Mungu ni kwa sababu wana mitazamo / fikra zao za kidemokrasia ambazo ziko tofauti kabisa na ufalme. Ni vigumu sana kwa waamini waliokulia kwenye demokrasia kuishi maisha ya ufalme,  Kwa sababu  Huwezi ukamtumikia Mungu na ukafaidi ahadi zake ukiwa na fikra za kidemokrasia.

 Zifuatazo ni baadhi tu ya tofauti zilizopo kati ya Ufalme wa Mungu na Demokrasia:-

1.  Ufalme wa Mungu umejengwa kwenye nguvu za Mfalme

Demokrasia imejengwa kwenye nguvu ya umma.

2.  Katika Ufalme wa Mungu  kuna kura moja tu, ya Mfalme. kiongozi ndiye anaye chagua raia au wafuasi wake ( “Si ninyi mlionichagua, bali Mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika Jina Langu, awape.” Yohana 15:16). Katiaka ufalme wa Mungu Raia hawaruhusiwi kuchagua kiongozi, kiongozi ndiye anaye chagua raia wake.

Katika Demokrasia raia wana haki ya kuchagua na kuteua viongozi wanaowataka.

3. Ufalme ni wazo la Mungu kutoka Mbinguni.

Demokrasia ni wazo la mwanadamu kutoka Ugiliki.

4.  Katika Ufalme wa Mungu, neno la Mfalme ni sheria. (“27 Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini’. 28 Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Mathayo 5:27 – 28) Mathayo 5:33-35, 43-44.

Katika Demokrasia, sheria inatungwa kutokana na maoni ya raia.

5.  Katika Ufalme wa Mungu, Mfalme anatawala.

Katika Demokrasia, wengi wanatawala.

6.  Katika Ufalme wa Mungu, kila raia anamtegemea mfalme ili akidhi matakwa yake (the people are dependent upon the King).

Katika Demoklasia, kila raia anafanya kazi kwa ajili ya kukidhi matakwa yake binafsi (independence).

7.  Katika ufalme Mfalme hawezi kuahidi jambo na asilitimize.( “22 Binti yake Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani.

Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.” 23Tena akamwahidi kwa kiapo akamwambia, “Cho chote utakachoomba nitakupa, hata kama ni nusu ya ufalme wangu.” 24Yule binti akatoka nje akaenda kumwuliza mama yake, “Niombe     nini Mama yake akajibu, “Omba kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 25Yule binti akarudi haraka kwa mfalme akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia. 26Mfalme akasikitika sana, lakini kwa sababu alikuwa ameapa mbele ya wageni wake hakutaka kumkatalia. 27Mara mfalme akatuma askari mmojawapo wa walinzi wake kukileta kichwa cha Yohana. Akaenda na kumkata Yohana kichwa humo gerezani, 28akakileta kichwa chake kwenye sinia na kumpa yule msichana, naye yule msichana akampa mama yake. 29Wanafunzi wake walipopata habari hizi, wakaja kuuchukua mwili wake, wakauzika kaburini.” Marko 6:17- 29)

Katika Demokrasia kiongozi anaweza akaahidi na asitimize ahadi yake.

8.   Katika ufalme wa Mungu, Mfalme anamiliki kila kilichomo katika himaya yake kuanzia raia, kila kiumbe, ardhi ,mimea, madini, vitu vyote vinakuwa chini ya umiliki wa mfalme. Ndiyo maana kila mfalme anaitwa BWANA maana neno BWANA(LORD) ni mmiliki(owner). (“Nchi ni mali ya BWANA pamoja na vyote vilivyomo ndani yake, Dunia nao wote wakaao ndani yake,”Zaburi 24:1).

Katika Demokrasia kiongozi wa nchi hana umiliki wa kitu chochote.

9. Katika ufalme wa Mungu  huwezi kwenda mbele za mfalme mikono mitupu, ni lazima uwe na chochote cha kupeleka mbele za mfalme kama zawadi. (kutoka 23:14c)

Katika demokrasia unaweza kwenda kwa Raisi mikono mitupu.

10.Katika ufalme , Mfalme anazaliwa kutoka katika ukoo wa kifalme.

Katika demokrasia  Raisi anachaguliwa kutoka katika ukoo  wowote kwa kupigiwa kura na raia.

11.Katika ufalme wa Mungu  Kila mtu hutafuta faida ya mwingine (preffering  others).(24 Mtu ye yote asitafute yaliyo yake mwenyewe, bali kila mtu atafute yale yanayowafaa wengine 1Korintho 10:24).

Katika demokrasia Kila mtu anatafuta faida yake binafsi (people competition).

12.Katika ufalme wa Mungu Katiba ya nchi inatokana na mawazo  / matakwa ya Mfalme  (“BWANA alipomaliza kusema na Musa juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vibao viwili vya Ushuhuda, vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu.”kutoka 31:18)  kutoka 20:1-17.

Katika demokrasia Katiba ya nchi inapatikana kutokana na maoni ya raia wake.

13.Katika ufalme Utajiri / mafanikio ni kwa kila raia (Commonwealth).

Katika demokrasia utajiri ni kwa mtu binafsi (private wealth).

14.Katika ufalme wa Mungu  huwezi ukaandamana kumpinga kiongozi aliyeko madarakani maana hukumchagua.

Katika demokrasia Raia wanaweza kuandamana na kumpinga kiongozi aliyeko

Madarakani wakimtaka ajiuzuru.

15.Katika ufalme wa Mungu Utawala wa mfalme hauna kikomo (16 BWANA ni Mfalme milele na milele, mataifa yataangamia watoke nchini mwake. zaburi 10:16).

Katika demokrasia utawala wa Raisi una kikomo .

16.Katika ufalme wa Mungu, raia wanamsifu na kumwabudu Mfalme, ndio utamaduni wao. (Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa zaburi 47:7).

Katika demokrasia raia hawana utamaduni wa  kumsifu na kumwabudu kiongozi wao.

By
Dawson Kabyemela,
Kingdom Influence Network.