MAMBO 5 MUHIMU YAKUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA MATHAYO 6 : 33

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa” ( Mathayo 6:33)

Kutokana na maneno haya ya Yesu Kristo, tunapata msingi ambao ukiuelewa na ukautumia, unaweza ukawa na maisha mazuri sana! Msingi huo ni huu: Tafuta kwanza ufalme wa Mbinguni na haki yake, na hayo yote unayoyatafuta katika maisha utapewa na kuzidishiwa.”

Note: When you seek first the Kingdom of God and His righteousness you become like a magnet attracting other things to you.

Ukisoma Mathayo 6:24-34 utaona ya kuwa Yesu alipokuwa anasema “na hayo yote mtazidishiwa” alikuwa na maana ya mavazi, vyakula na mahali pa kulala. Kwa tafsiri iliyo laini na nyepesi ya Mathayo 6:24-34,Yesu Krsito alitaka watu wake tujue ya kuwa,Mfumo wetu wa maisha na matokeo ya kuishi kwetu, kunaonyesha ya kuwa kuna kitu ambacho mioyo yetu inakitafuta. Inaonyesha ya kuwa mipangilio ya vipaumbele vya maisha yetu,kuna kitu tunachokitafuta tena baada ya kuona ya kuwa tumekipoteza.

MAMBO 5 YAKUJIFUNZA

  1. Mpangilio wa vipaumbele (priorities) vyetu vinavyosukuma utafutaji wetu wa maisha umekosewa. Tulitakiwa tutafute kwanza ufalme wa Mungu.
  2. Tunachokitafuta sicho chenyewe ambacho mioyo yetu ilikipoteza katika maisha. Kwa hiyo mioyo yetu inabaki kusumbukia(worry) maisha haya,kwa kuwa haipati kile ambacho hasa ndicho inachokitafuta.
  3. Kwa kuwa vipaumbele vya maisha yetu havijalenga kupata hasa kile tunachotakiwa kukipata,…mioyo yetu bado inadai kuendelea kuhangaika kutafuta hata baada ya kupata kile tulichofikiri kitaridhisha mioyo yetu baada ya kukipata…na kumbe si chenyewe.
  4. Matokeo ya mipangilioo ya vipaumbele vya utafutaji wetu, ni kuwa na maisha ya kitumwa na ya kujisumbua na ya mahangaiko,na yaliyojaa hofu ya kesho itakuwaje?!
  5. Tunatafuta maisha kwa kuwa tunadhani tulipoteza maisha wakati hatukupoteza maisha, bali tulipoteza ufalme wa Mungu ambamo ndani yake kuna maisha tunayoyatafuta.

Kwa hiyo ikiwa unatafuta maisha mazuri, nakushauri kama Yesu alivyosema, usitafute maisha mazuri, bali tafuta kwanza ufalme wa Mungu utapata maisha unayoyatafuta.

Amen!

© Mwalimu D. R. Kabyemela

© 0714 606 500 / 0757 263 226

© Ufalme wa Mungu Kwanza

© www.kinet.org/umk

© www.kinet.org

© U M K

Leave a Reply