MAMBO 15 MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU UFALME WA MUNGU

UTANGULIZI

Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu sisi wanadamu tulikuwa tunaishi MBINGUNI na Mungu ( Efeso 1 : 4 ), kipindi hicho tulikuwa hatujapewa miili na kuletwa hapa duniani, tulikuwa ni roho. Mtu ni roho inayoishi kwenye nyumba inayoitwa mwili. Ndiyo maana ukifa watu wanasema huu ni mwili wa marehemu, ikiwa na maana kwamba mwenye mwili hayupo umebaki mwili wake.

MBINGUNI ni nchi iliyopo katika ulimwengu wa roho, ulimwengu wa roho ni mahali ambapo roho zinakaa. Mbinguni ni nchi yenye utawala wa kifalme kama vile Tanzania ilivyo nchi yenye utawala wa ki-demokrasia, unaposoma kwenye Biblia katika kitabu cha WAEBRANIA 11:15-16 maneno ya Mungu yanasema hivi:- “15 Kwa kweli kama wangekuwa wanafikiri kuhusu NCHI waliyoiacha, wangalipata nafasi ya kurudi huko. 16 Lakini badala yake wanatamani NCHI ILIYO BORA ZAIDI, YAANI, NCHI YA MBINGUNI. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa amekwisha kuandalia mji kwa ajili yao”.

SABABU ZA MUNGU KUIUMBA DUNIA NA KUMWEKA MWANADAMU
Ni utaratibu wa nchi za kifalme kwamba baba akiwa ni mfalme akafa anamwachia madaraka mwanae wa kwanza wa kiume kwa ajili ya kuendelea kutawala nchi hiyo, kumbuka sisi ni wazaliwa wa kwanza na Mungu ni Baba yetu. (Waebrania 12 : 23)

Mungu kama Baba yetu yeye anaishi milele hafi. Sasa alipoona yeye utawala wake ni wa milele hawezi kufa na huku anataka watoto wake watawale ndo maana aliamua kututafutia koloni ambalo ni dunia ili sisi kama watoto wake tutawale duniani na yeye aendelee kutawala Mbinguni. ( Mwanzo 1 : 26 , zaburi 115:16, Ufunuo 5:9-10, 1:6, Kutoka 19:6).

Tunapozungumza kuhusu UFALME WA MUNGU hatuzungumzii dini bali Ufalme wa MBINGUNI ambapo Mungu anakaa, watu wengi wanachanganya ufalme wa Mungu na dini. Dini ni mifumo iliyoanzishwa na wanadamu kwa ajili ya kumtafuta Mungu au miungu, lakini UFALME WA MUNGU ni mfumo wa utawala.
UFALME WA MUNGU makao yake makuu ni nchi ya MBINGUNI ndiyo maana hata wakati mwingine huwa tunasema Ufalme wa Mbinguni badala ya UFALME WA MUNGU.
Kwa hiyo Mbinguni ni nchi iliyopo katika ulimwengu wa roho na utawala wake ni wa kifalme ndiyo maana Mungu ni mfalme wala siyo Raisi.


Kwa leo tuishie hapa tutaendelea kesho na sehemu ya kwanza,

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza
© www.kinet.org/umk
© info@kinet.org
© U M K

Leave a Reply