JINSI SHETANI ANAVYOTUMIA HOFU KUKUANGAMIZA

Ayubu 3 : 25 “ Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo HOFU hunijilia”.

Shetani kwa asili alishashindwa asilimia mia moja na wana wa Mungu. Lakini yeye anachokifanya anatumia SIRAHA YAKE INAYOITWA HOFU ili kukuangamiza.

Kuna watu wanaogopa kuibiwa na matokeo yake wanaibiwa kila mara, kuna watu wanaogopa wachawi na matokeo yake wanalogwa kila siku, kuna watu wanaogopa magonjwa na matokeo yake magonjwa hayaishi kwao, wengine HOFU yao ni kuachwa kwenye mahusiano na wengine HOFU yao ni kifo.

Shetani anaijua na anaitumia sana kanuni hii ya kwamba chochote kinachokutia HOFU ni lazima ukipate, hivyo kuwa makini na HOFU zako.

Shetani anaweza kukuletea ndoto ya kukutia HOFU ili UOGOPE. Katika kitabu cha Ayubu imeandikwa “……hunitia HOFU katika ndoto……..”. Na kwa kanuni ya HOFU, lile jambo unalolihofia ndilo linalokupata. (Ayubu 3:25).

Kimsingi shetani anapokuletea ndoto ya hofu, anataka ukiamka uanze kuhofia ile ndoto uliyoiota. Anataka uwe na HOFU ili ukipata HOFU jambo hilo likupate.

Nakujulisha, MWANA WA UFALME unapoota jambo la kutisha, unapoamka uwe na Neno kinywani mwako. Sema kwa jina la Yesu hii ndoto mbaya haitanipata mimi hata siku moja kwa jina la Yesu.

Unaweza kuumba kile unachokihofia na shetani anaijua kanuni hii ya kuwa lile unalolihofia ndilo linalokupata. Ndio maana kwenye Biblia neno USIOGOPE limeandikwa mara 366.

MUNGU ANAJUA NJIA PEKEE YA SHETANI KUKULETEA MAANGAMIZI NI KUKUOGOPESHA KWA KUTUMIA NDOTO AU MATUKIO MBALIMBALI.

Shetani anaweza pia kukuogopesha kwa kutumia watu ambao wanankuja kuongea na wewe mpaka unaogopa, au taarifa za kwenye vyombo vya habari zinazotia HOFU.

Ukifatilia sana vyombo vya habari utashangaa taarifa nyingi ni taarifa zinazotia HOFU, hata mazungumzo ya watu wengi ni mazungumzo yanayotia HOFU, utasikia mara “dunia hii imekwisha, yaani maisha ya sasa hivi ni magumu sana, hakuna hela, inavyoonekana kuna kuna hili kuna lile, yaani matatizo kibao”.

Hapo shetani anataka atumie nafasi hiyo kukutia HOFU maana anajua yeye alishashindwa, isipokuwa HOFU YA MAUTI ndio inatenda kazi ndani yetu. Anataka kukutia HOFU.

Ndio maana sasa Mungu na yeye akajua kwamba neno usiogope litatenda kazi. Na kwa sababu hiyo limeandikwa ndani ya Biblia mara 366, ina maana kuwa kila siku Yesu anakwambia USIOGOPE.

Na mimi leo nakwambia USIOGOPE kwenye biashara, USIOGOPE kwenye kazi, USIOGOPE kwenye ndoa, USIOGOPE wezi, USIOGOPE wachawi, USIOGOPE magonjwa, USIOGOPE kifo, USIOGOPE, USIOGOPE, USIOGOPE. Kwa jina la Yesu, Amina.

Asante na Mungu akubariki sana.

© D. R. Kabyemela

© 0714 606 500

© Ufalme wa Mungu Kwanza

© www.kinet.org/umk

© info@kinet.org

© U M K

6 thoughts on “JINSI SHETANI ANAVYOTUMIA HOFU KUKUANGAMIZA

 1. Hello. I see that you don’t update your page too often. I know that writing content is
  time consuming and boring. But did you know that there is
  a tool that allows you to create new posts using existing content
  (from article directories or other websites from your niche)?
  And it does it very well. The new articles are high quality and
  pass the copyscape test. Search in google and try: miftolo’s
  tools

 2. Hi. I have checked your kinet.org and i see you’ve got some duplicate content so probably it is the reason that you don’t rank high in google.
  But you can fix this issue fast. There is a tool that rewrites
  content like human, just search in google: miftolo’s tools

Leave a Reply