UHURU WA KULA MATUNDA YA KILA MTI (Freedom of access)

Mwanzo 2:16
Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

And the LORD God commanded the man, “You are free to eat from any tree in the garden;

Mungu alipomuumba mwanadamu na kumuweka kwenye bustani ya Edeni( uwepo wa Mungu) alimpa uhuru wa kula matunda ya kila mti (freedom of access), lakini hakumpa umiliki (ownership).

Hii ina maana gani kwenye UFALME WA MUNGU, chochote ulichonacho ambacho Mungu amekupa una uhuru wa kukitumia kwa ajili yake lakini huna umiliki wake.

Biblia iko wazi kabisa ,
” Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake “.
Zaburi 24:1.

Bwana == Lord == Owner

Kila ulichonacho ni mali ya Bwana (Owner), liwe ni gari, nyumba, fedha, watoto, mke, mume au mali yoyote ni mali ya Bwana yeye ndiye mmiliki wewe umepewa kutunza kwa niaba ya Mungu una uhuru wa kutumia unavyotaka lakini huna umiliki wake ndiyo maana hata ukifa vyote unaacha.

Umaskini wa mwanadamu unaanzi pale anapoanza kufikiri kuwa kila alichonacho ni chake.

Watu wengi ni wagumu sana kutoa sadaka pale Mungu anapodai sadaka bila kujua wanaye mnyima sadaka ndiye mwenye mali.

Sisi kama wana wa Ufalme tunatakiwa tutambue kwamba kila tulichonacho ni mali ya Mungu.

NB: In the Kingdom of God you are free to access anything but you own nothing.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Dawson. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza
© Whatsapp 0714 606 500
© www.kinet.org/umk
© info@kinet.org
© Mathayo 6:33
© U M K

Leave a Reply