MAMBO 15 MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU UFALME WA MUNGU.

JAMBO LA NANE : KODI YA MUNGU – ( ZAKA )

Malaki 3:8-10

8 Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia. ‘‘Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’ ‘‘Mnaniibia ZAKA(mnaniibia kodi) na dhabihu. 9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 10 Leteni ZAKA kamili (leteni KODI kamili) ghalani , ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la.”

Kwenye UFALME WA MUNGU kuna mfumo wa ulipaji wa KODI. Sisi kama raia wa ufalme wa Mungu, tunatakiwa kulipa KODI ( ZAKA / FUNGU LA KUMI ) kwa sababu KODI ( ZAKA ) ndiyo inayosaidia katika uendeshaji wa shughuli za UFALME WA MUNGU hapa duniani.

FUNGU LA KUMI au ZAKA kwa RAIA WA UFALME WA MUNGU si swala la hiari, NI SHERIA NA LAZIMA. FUNGU LA KUMI ni KODI YA MUNGU. Mungu Anachukua 10%  ya kila anachokupatia, wewe unabaki na 90% lakini bado RAIA wengi wamekuwa wakimuibia Mungu KODI yake. Kwenye kitabu cha MALAKI 3:8-11 Mungu anawaita wote wasiotoa FUNGU LA KUMI ( KODI ) kuwa ni wezi.

FUNGU LA KUMI ni njia ya kibiblia na kanuni ya UFALME WA MUNGU INAYOTUMIWA NA MUNGU KUIENDELEZA [ KUI-SUPPORT] kazi yake na shughuli za ufalme wake, kazi ya UFALME WA MUNGU inasuasua kwa sababu RAIA wengi wa MBINGUNI hawalipi KODI ( FUNGU LA KUMI ).

FUNGU LA KUMI  ni njia ya Mungu kuwatunza watumishi wake/ makuhani na walawi (watumishi kwa ujumla). Hebu fikiria mtumishi wa Mungu anayekulisha wewe vya rohoni, ambaye anakaa miguuni kwa BWANA kutafuta majibu ya maisha yako, ambaye ni FULL TIME MINISTER, Unataka ale wapi? Mungu ameweka FUNGU LA KUMI kama sehemu yao ya kuendeshea maisha yao. Je ingekuwaje Mchungaji wako aache kuomba na kusimamia kazi ya Mungu naye atafute pesa na maisha kama wewe, hasara ngapi utapata na kwa kiasi gani Mungu na Ufalme wake utapata shida? Ndio maana kati ya vitu ambavyo SHETANI ANAPIGIA KELELE SANA KUPITIA VINYWA VYA WATU NI FUNGU LA KUMI.

FAIDA ZA KULIPA KODI –  ( KUTOA FUNGU LA KUMI )

MALAKI 3:8-11 Mungu anaeleza wazi FAIDA NA UMUHIMU WA KUTOA FUNGU LA KUMI/ ZAKA ( KODI ), NAZO NI;

  1. Unamuweka Mungu kazini kulinda uchumi wako na mfumo wako wa kifedha.
  2. Kupitia fungu la kumi unafanya agano na Mungu, na unajenga ushirika na kuliweka kumbukumbu lako mbele za Bwana
  3. Unamfungulia Mungu mlango na njia ya kupitishia baraka zake za mjini na mashambani ili azijaze hazina zako hata isiwepo nafasi ya kutunza baraka hizo.
  4. Unamweka Mungu kazini kushughulika na maisha yako na ya watu wako.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela

© Ufalme wa Mungu Kwanza

© www.kinet.org/umk

© info@kinet.org

© U M K