MAMBO 15 MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU UFALME WA MUNGU.

JAMBO LA NNE : LUGHA YA MBINGUNI.

Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa LUGHA mpya; ( Marko 16 : 17 ).

Biblia sio kitabu cha kidini kwasababu imebeba Agano. Agano maana yake ni (mkataba). Biblia ina Agano la Kale na Agano Jipya. Unapokuwa unafungua Biblia utakutana na Agano la kale na Agano Jipya. Biblia ni kitabu cha kisheria. Ni hati ya kisheria, ni mkataba wa kisheria hivyo sio kitabu cha dini. Biblia ni sheria.

“Serikali hii ya kifalme imetoa ahadi zake kwenye katiba kwa wana wa Ufalme ambao ni sisi tuliomkiri Mfalme Yesu kuwa mmiliki wetu ndani ya ufalme wa mbinguni hapa Duniani”

Biblia inahusu nchi inayoitwa Mbinguni.
Sisi ni koloni la nchi hiyo hapa duniani.

LUGHA YA MBINGUNI

Kila nchi ina LUGHA yake ya taifa, vile vile MBINGUNI ni nchi ambayo ina LUGHA yake. KUNENA KWA LUGHA ndiyo lugha ya taifa katika UFALME WA MUNGU.

Kuna lugha za malaika ( Mbinguni ) au mapepo ( Kuzimu ) na lugha za wanadamu (Duniani ), ndiyo maana ukienda kwa mganga wa kienyeji mashetani yakipanda juu yake hata lugha inabadilika anaanza kuongea lugha ya Mashetani ( Kuzimu ).

LUGHA ni chombo kikuu cha mawasiliano, mawasiliano ndiyo yanayojenga mahusiano, mwanadamu alipopoteza mahusiano yake na Mungu akawa amepoteza LUGHA YA MBINGUNI, ujio wa Yesu Kristo Duniani ulikuwa ni kurudisha mahusihano kati Mungu na mwanadamu, ndiyo maana mtu anapomwamini Yesu jambo la kwanza analopewa ni LUGHA ya Mbinguni maana imeandikwa “ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa LUGHA mpya;”  ( Marko 16 : 17 ).

LUGHA ndiyo nguvu ya taifa, ndiyo maana hata siku ile ya Pentekoste Roho Mtakatifu aliposhuka jambo la kwanza alilofanya ni kuwapa LUGHA mpya wale wanafunzi. (Matendo ya mitume 2:1-4 ).

KUNENA KWA LUGHA ni roho yako inawasiliana na Mungu Moja kwa moja hata akili yako inakuwa haielewi, KUNENA KWA LUGHA ni lugha pekee ambayo Shetani haelewi unachoongea.

Unapoomba kwa Lugha kumbuka sio wewe ni Roho Mtakatifu. Maombi ya moja kwa moja kwa Mungu

Warumi 8:26 Hatujui jinsi ya kuomba, Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa

1 Korintho 14:2 Kunena kwa Lugha unaongea na Mungu, unamwambia Mungu mambo ya siri kutoka rohoni mwako.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela

© Ufalme wa Mungu Kwanza

© www.kinet.org/umk

© info@kinet.org

© U M K