Mathayo 21 : 21 – 22
21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na IMANI, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. 22 Na yo yote mtakayoyaomba katika sala MKIAMINI, mtapokea.

Mwanadamu amekuwa ni kiumbe pekee aliyeumbwa na Mungu ambaye anaishi maisha magumu, ya kuangaika na kutapatapa hapa duniani kwa sababu ya kukosa maarifa ya ufalme wa Mungu.

UFALME WA MUNGU ni kipaumbele cha kwanza cha Mungu kwa kila mwanadamu, Mungu anasisitiza kila mwanadamu kuutafuta kwanza Ufalme wake na haki yake kabla ya jambo lolote ( Mathayo 6:33). Kutafuta ni pamoja na kujifunza ili upate ufahamu.

Jambo la tatu na la muhimu kujua kuhusu UFALME WA MUNGU ni MATUMIZI YA IMANI KWENYE UFALME WA MUNGU.

Mbinguni ni nchi ambayo kama nchi zingine ina chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma kati ya raia wake, na chombo hicho ni IMANI. Kama ilivyo katika maisha ya kawaida ya hapa duniani, ili uweze kupata huduma au bidhaa yoyote ni lazima utoe fedha, vile vile katika ufalme wa Mungu pasipo IMANI huwezi kupata chochote kutoka kwa Mungu.

NOTE: In the spiritual realm FAITH is the CURRENCY that man exchanges for things of value in God’s Kingdom such as salvation, healing, deliverance, peace, prosperity, etc.

Every promise made to man in the Bible is capable of being received in exchange for FAITH.

Ufalme wa Mungu ni nchi ambayo fedha yake ni IMANI. Huwezi kupata chochote katika ufalme wa Mungu bila ya kuwa na IMANI. Kama vile ambavyo huwezi kuishi katika nchi yoyote duniani na kupata mahitaji yako ya kila siku bila ya kuwa na fedha, vilevile huwezi kuishi katika ufalme wa Mungu na kupata mahitaji yako yote bila ya kuwa na IMANI.

Kuna wakati unaweza kutamani kununua simu ya Tshs 200,000 wakati wewe mfukoni una Tshs 50,000 tu, ukienda dukani utaambiwa haiwezekani, ongeza pesa, utaambiwa hizo pesa ni pungufu.

Kuna siku wanafunzi wa Yesu walitaka kutoa huduma, halafu wakashindwa, Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza ??, Na Yesu aliwajibu hivi;

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa IMANI yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na IMANI kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. ( Mathayo 17 : 20 )

Kama ilivyo katika ulimwengu wa mwili wale ambao hawana hela tunawaita maskini, vile vile katika ulimwengu wa roho wale ambao hawana imani ni masikini wa rohoni.

EBU FIKIRI; unapokwenda dukani kununua sukari lazima uende na pesa maana unajua mahitaji ya sukari kwa mwenye duka yanaambatana na pesa, na bila kutoa pesa kwa mwenye duka sukari hupati. Vile vile maombi ambayo hayaambatani na IMANI hayajibiwi. ( Yakobo 1 : 5 – 7 )

Kumbuka hili, chanzo cha IMANI ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo ( Warumi 10 : 17), hivyo jitahidi sana kusikia Neno la Kristo ili uongeze kiwango chako cha IMANI.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza
© www.kinet.org/umk
© info@kinet.org
© 0714 606 500
© U M K