MAMBO 15 MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU UFALME WA MUNGU.

JAMBO LA TANO : MWANASHERIA MKUU WA MBINGUNI.

Luka 12:11-12

 Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12 Kwa maana ROHO MTAKATIFU atawafundisha wakati uo huo mnachopaswa kusema.”

 Kabla ya wakoloni kuja kuitawala Afrika kwanza walituma vitangulizi vya ukoloni ambavyo vilikuwa ni Wapelelezi, Wafanyabiashara na Wamissionari. Huu ni utaratibu wa kawaida, kabla koloni halijaanzishwa mahali ni lazima pawepo na vitangulizi vya koloni.

Hata kabla ya Yesu kuja na ufalme wake hapa Duniani, alikuwa na mtangulizi wake Yohana Mbatizaji ( Yohana Mbatizaji ni kitangulizi cha ukoloni – Yohana 3 : 4 ), mtangulizi anakuja kuitengeneza njia kwa ajili ya mfalme anayekuja nyuma yake.

Kabla ya Mungu kuanzisha koloni lake hapa duniani ilibidi atume kitangulizi cha ukoloni ambaye ni ROHO MTAKATIFU – Mwanzo 1 : 2, kwa hiyo ROHO MTAKATIFU ni kitangulizi cha ukoloni wa Mbinguni hapa duniani.

ROHO MTAKATIFU ana kazi nyingi sana kwenye UFALME WA MUNGU , ususani kwenye kipindi hiki cha siku za mwisho maana Mungu alisema atamwaga Roho wake juu ya watu siku za mwisho. Hiki ni kipindi cha ROHO MTAKATIFU,  maana Mungu alitangulia halafu akaja Yesu na sasa ni nafasi ya ROHO MTAKATIFU kwetu.

NOTE: HOLY SPIRIT is The Most Important Person on Earth, HOLY SPIRIT is the Governor of God’s kingdom on earth.

MWANASHERIA MKUU WA MBINGUNI.

Mbinguni ni nchi ambayo ina mwanasheria wake ambaye ni ROHO MTAKATIFU, ROHO MTAKATIFU ana kazi nyingi sana kwenye UFALME WA MUNGU ikiwa ni pamoja na kazi ya kuwa mwanasheria

ROHO MTAKATIFU ni mwanasheria mkuu wa MBINGUNI, yeye ndiye aliyehusika katika uandikaji wa katiba (Biblia) 2:Petro 1:20-21.

ROHO MTAKATIFU kama mwana sheria mkuu katika UFALME WA MUNGU, yeye ndiye anayehusika katika kuwaongoza na kuwafundisha RAIA wa UFALME WA MUNGU jinsi ya kusema wanapopelekwa mbele ya mabalaza na mahakama au masinagogi, unaposoma kitabu cha Luka 12:11-12 neno la Mungu linasema hivi:- „„Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12Kwa maana ROHO MTAKATIFU atawafundisha wakati uo huo mnachopaswa kusema.”

Unapokwenda mbele za Mungu kuomba kwa ajili ya kudai haki yako, kuna namna ya kujieleza, ukishindwa kujieleza vizuri haki yako hupati. Isaya 43 : 26  Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Prayer is not begging God, PRAYER IS PETITION ( maombi ni madai ).

Kazi kubwa ya ROHO MTAKATIFU kama mwanasheria mkuu wa Mbinguni yeye ndiye anayekusaidia wewe raia wa Mbinguni ili uweze kujieleza vizuri na kupata / kupewa haki yako, Warumi 8:26 Hatujui jinsi ya kuomba, Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Kwa leo naomba niishie hapa, nakutakia siku njema, uende ukafanye mambo makubwa na yasiyo ya kawaida maana wewe siyo wa kawaida.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela

© Ufalme wa Mungu Kwanza

© www.kinet.org/umk

© info@kinet.org

© U M K