20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, UFALME WA MUMGU utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, UFALME WA MUNGU hauji kwa kuuchunguza; 21 wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, UFALME WA MUNGU umo ndani yenu.

Unapoingia katika UFALME WA MUNGU jambo la kwanza ambalo Mungu anaanza kushughulika nalo kwako ni kubadili jinsi ya kufikiri kwako, kwa sababu hakuna chochote kile kinachoweza kubadika ndani ya maisha mwanadamu mpaka amebadili jinsi ya kufikiri kwake (nothing can change in your life until you change in your mind ).

Ndiyo maana BWANA Yesu alipoanza kuhubiri alisema hivi :- TUBUNI: kwa maana UFALME WA MBINGUNI umekaribia, Toba (Repent – change in your mind – change your operating system, change your belief system, change the way you think, to think differently) badili mfumo wa fikra zako.

UFALME WA MUNGU ni program ambayo Mungu aliitengeneza na kuiweka ndani ya mwanadamu ili Mungu aweze kutumia fikra (Mind) za mwanadamu na kutimiza mapenzi yake duniani. Ndiyo maana Yesu alipoulizwa na Mafalisayo UFALME WA MUNGU utakuja lini, Yesu alisema hivi “UFALME WA MUNGU umo ndani yenu” (Luka 17:20 – 21)


UFALME WA MUNGU ni kama operating system ndani ya kompyuta ambayo Mungu aliiweka ndani ya mwanadamu na anaitumia ili kutimiza mapenzi yake hapa duniani yeye akiwa mbinguni, kumbuka ya kwamba na shetani naye anatumia fikra(Mind) za mwanadamu kutimiza mapenzi ya ufalme wake duniani.

Mungu anapotaka kutimiza mapenzi yake hapa duniani ni lazima atumie fikra za mwanadamu, na shetani hivyo hivyo. Mapenzi ya Mungu yanatimizwa kupitia mfumo wa ufalme wa Mungu unapokuja katika fikra zetu, ndiyo maana wanafunzi wa Yesu walipo muuliza jinsi ya kusali alisema hivi:- Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye Mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbunguni (Mathayo 6:9 – 10)

Dhambi inapoingia katika maisha ya mwanadamu inasababisha program ya Mungu inayoitwa UFALME WA MUNGU iharibike(corrupt)- kutoka 32:7.

Dhambi ni kirusi kinachoingia katika maisha ya mwanadamu na kuharibu program za Mungu zilizomo katika fikra za mwanadamu.

Damu ya Yesu ni software (antvirus) inayosafisha dhambi (virus) ndani ya mwili wa mwanadamu ili Roho mtakatifu aishi ndani ya mwanadamu huyo.

Dhambi ilipoingia duniani, program ya Mungu aliyoiweka ndani ya mwanadamu inayoitwa UFALME WA MUNGU iliharibika (corrupt) ,

Hivyo mwanadamu akapoteza connection kati yake na Mungu na mahangaiko ya mwanadamu yakaanzia pale, mwanadamu akaanza kutapatapa kama samaki atapatapavyo pindi aondolewapo majini mpaka sasa bado mwanadamu anatapatapa, mwanadamu bado ananyauka kama mmea uliongolewa kwenye ardhi, mwanadamu mpaka sasa hajui alipoteza nini na anahangaikia nini.

Kila mwanadamu anahitaji UFALME WA MUNGU kama vile samaki anavyo hitaji kuishi majini kwa sababu ndiyo mazingira yake.

Ili mwanadamu apate utulivu, amani, furaha ya kudumu anahitaji UFALME WA MUNGU tofauti na hapo mwanadamu ataishi maisha ya wasiwasi na mahangaiko mpaka kufa kwake.

NOTE: You did not created to live without your creator (GOD), otherwise you will struggle to live.

Nakutakia siku njema, uende ukafanye mambo makubwa na yasiyo ya kawaida maana wewe siyo wa kawaida.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela
© Ufalme wa Mungu Kwanza
© www.kinet.org/umk
© info@kinet.org
© U M K