MAMBO 15 MUHIMU UNAYOPASWA KUJUA KUHUSU UFALME WA MUNGU.

JAMBO LA SITA : WAKILI WA SERIKALI YA MBINGUNI.

Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, YESU KRISTO Mwenye haki.

1Yohana 2:1

My dear children, I write this to you so that you will not sin. But if anybody does sin, we have an ADVOCATE with the Father JESUS CHRIST, the Righteous One. 1 John 2 (NIV)

Leo tunaaangalia jambo la sita unalopaswa kujua kuhusu UFALME WA MUNGU ambalo ni WAKILI ( ADVOCATE ) wa serikali ya Mbinguni.

WAKILI(MWANASHERIA)

Leo tunaaangalia jambo la sita unalopaswa kujua kuhusu UFALME WA MUNGU ambalo ni WAKILI ( ADVOCATE ) wa serikali ya Mbinguni.

Katika serikali ya Mbinguni YESU KRISTO ana kazi nyingi sana, kati ya kazi hizo ni pamoja na kazi ya UWAKILI.

YESU KRISTO ndiye WAKILI ( ADVOCATE ) wa serikali ya MBINGUNI

Naamini WAKILI wamjua.
Wakili husimama kujibu kesi badala ya mwenye kesi. Awe na hatia au asiwe na hatia. Wakili hukaa kwenye nafasi ya mwenye kesi na kujibu maswali yote kwa NIABA ya mwenye kesi. Wengine humwita “mwanasheria”.

Mawakili husimama katikati ya mshtaki na mshtakiwa. Hupokea lawama au pongezi zote kwa NIABA ya mwenye kesi na wakati wakili akiongea, muwakilishwa huwa kimya kabisa. Anakuwepo mahakamani lkn hasemi lolote. Wakili wake husema kwa niaba yake.

Ili upate huduma ya wakili, kwanza unaongea naye kuhusu kesi yako. Unamwambia kweli yote. Kweli tupu. Hata kama umeua. Ndipo mtakubaliana jinsi ya kuenenda na kesi. Kesi huendeshwa kisheria, wakili ni mjuzi wa sheria.

YESU KRISTO kama WAKILI wa serikali ya Mbinguni yeye usimama na kututetea mbele za Mungu ( Hakimu ) baada ya sisi kumwambia mahitaji na matatizo yetu.

Yesu ni mtetezi ( WAKILI / ADVOCATE ) wetu mwambie mwambie shida na matatizo yako ili akutetee mbele za Mungu ( Hakimu ).

NAOMBA NIKUTAHADHARISHE UNAPOFANYAKAZI NA YESU KAMA WAKILI

Ukisoma Waebrania 4 : 14 Neno la Mungu linasema hivi
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.

Hakikisha unashikilia kile ulichomwambia YESU kama WAKILI wako, mfano unaumwa presha, halafu unamwambia YESU akutetee upate haki yako ya uponyaji, ili YESU aendelee kukutetea na wewe unatakiwa uendelee kukiri uponyaji wa hiyo presha. Acha mambo ya kuendelea kusema jamani hii presha yangu. Unamnyima nguvu WAKILI ya kuendelea kukutetea.

Yapo mengi ya kuelezea kuhusu WAKILI ( ADVOCATE ) ila kwa leo naomba niishie hapa, nakutakia siku njema, uende ukafanye mambo makubwa na yasiyo ya kawaida maana wewe siyo wa kawaida.

Asante na Mungu akubariki sana.

© Mwalimu D. R. Kabyemela

© Ufalme wa Mungu Kwanza

© www.kinet.org/umk

© info@kinet.org

© U M K