VIPAWA NA VYOTA – Bishop Josephat Gwajima

Neno KIPAJI linaweza kuwa Karama au Kipawa.

KIPAJI huwezi kusomea ili ukipate, bali ni kitu ambacho unakua umepewa na Mungu kikufanikishe kwenye maisha yako.

Mithali 18:16

Kipaji alichonacho mtu humpatia nafasi na kumleta mbele za wakuu. Duniani kuna vitu ambavyo mtu anavipata lakini si kwa sababu ya elimu yake hata kama ana PhD. Ni rahisi kuendeleza kile kitu ambacho mtu amezaliwa nacho kuliko kumsomesha mtu afanye kitu ambacho hajazaliwa akifanye. Kipaji ni kitu ambacho Mungu amempangia mtu tangu kuzaliwa ili afanikiwe.

Mithali 17:8

Zaburi 45:12

Kuna watu hawana vipaji wana ambavyo vimewapa mali na mafanikio bila kwenda shuleni.

Kipaji ni ile nyota aliyozaliwa nayo mtu, na ndio maana elimu haimuhakikishi mtu mafanikio bali elimu ni taa inayomuongoza mtu kuyasaka mafanikio yaliyogubikwa na giza la ujinga. Mtu hahitaji kuwa na elimu ili afanikiwe, bali kile kipawa alichonacho mtu ndicho kinampeleka mtu na kufikia mafanikio yake na malengo ya moyo wake.

Mathayo 2:1-

Kuna wataalamu wa kusoma nyota, ambao wanaweza kusoma na kuona nyota ya mtu ndio maana Yesu alipozaliwa Mamajusi wa Mashariki waliiona nyota yake wakaifuata.

Yesu ni Mungu lakini alikua ana nyota yake alipozaliwa na hii inatufundisha kwamba:-

– Kila mtu ana nyota yake.

– Nyota ya mtu inaweza kufuatwa kwa ubaya au kwa uzuri.

– Nyota ya mtu inaweza kuonekana.

– Nyota ya mtu ikionekana unaweza kufuatwa.

– Nyota inaweza kuwaongoza watu mpaka ulipo.

– Nyota ikionekana utajiri unakufuata.

Kuna watu wengine nyota zao zipo ousoni, ukimwangalia tu unatamani uzungumze naye tena na tena, wengine nyota zao ni kwenye tumbo akizaa anazaa viongozi, wafanya biashara wakubwa na wachungaji n.k. Wengine nyota zao ni kwenye macho ana macho ya kuona fursa, na wengine nyota zao ni masikio kusikia habari njema, wengine nyota zao ni kwenye akili wanauwezo wa kupanga mipango ya fedha na fursa ndivyo Mungu amewaumba wanadamu kila mtu na nyota yake.

Sio kila mtu anaweza kufanya biashara akafanikiwa, kuna watu wana nyota za biashara lakini wao hawajijui.

UCHAWI

Kwenye maisha kuna watu wasiokupenda hata kama ukiwalisha kila siku; kama ni kwasababu ya wivu tu.

Wewe una nyota ya biashara umepewa na Mungu lakini hujui mchawi ana uwezo wa kuiona na kuichukua nyota yako akampa mtu ambaye hana nyota hiyo, na atakapokwenda mtu kwa mganga na kusema anataka nyota afanikiwe kibiashara ndio anawekewa nyota yako na anafanikiwa kwa sababu ya nyota iliyoibiwa kutoka kwa mtu mwingine.

Unakuta mtu amepewa pete au cheni lakini na ndani ya hiyo pete au cheni kunakuwa na nyota za watu ambazo zinamfanya anaanze kufanikiwa na yule aliyeibiwa nyota anaanza kuharibikiwa na kupatwa na magonjwa.

Mafanikio kwenye maisha sio magari na majumba na pesa, mafanikio ni kutimiza lile kusudi la Mungu lililokuleta duniani.

Mtu mwenye wivu anaweza kwenda kwa mganga na kumuomba amfunike mtu mwenye nyota ya kupendwa au mvuto. Mganga anaweza kuyatuma majini yakamfunika mtu mwenye tabia nzuri na nyota yake ikaibiwa abaki aonekane hafai. Majini au mashetani haya yanamdidimiza mtu huyo anabaki hawezi kufanya kitu chochote.

Luka 13:10

Mtu aliyeibiwa nyota hua mgonjwa na mwenye matatizo siku zote.

Mathayo 9:22

Siku moja mtu mmoja akamleta mwanae kwa Yesu, akamwambia mwalimu mwanangu ana pepo wa kifafa, (kifafa kinahusiana na akili) maana yake wachawi wameona mtoto yule ana nyota ya akili wakamwekea kifafa na kuchukua nyota yake ili abaki amedidimizwa na kushindw akutumia akili yake kupata mafanikio.

Watu wanaloga mpaka nchi, Tanzania ni nchi nzuri kweli kuishi, kusoma na ina fursa

nyingi za ardhi na malighafi lakini akili za baadhi ya watu zimefunikwa hawazioni fursa wamebaki wanalalamika sababu ya nyota zimeibiwa.

Yoeli 2:21

Ninaamuru nyota yako irudi kwa jina la Yesu uamke uzione fursa na kuzitumia sawasawa na nyota ya kipawa chako ili ufanikiwe kwa jina la Yesu.

One thought on “VIPAWA NA VYOTA – Bishop Josephat Gwajima

  1. Pingback: solars.biz

Comments are closed.